Saturday, 3 August 2019

WITO WA KUJIUNGA KATIKA USAILI WA NAFASI ZA KAZI IDARA YA UHAMIAJI

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linatangaza wito wa kujiunga na usaili wa nafasi za kazi katika Idara ya Uhamiaji kwa wahitimu wa mafunzo ya JKT kundi la kujitolea operesheni Kikwete na Operesheni Magufuli waliopo katika makambi ya JKT na wale waliokwishamaliza mkataba na kurudi majumbani kwao.
Vijana hao wanatakiwa kuripoti katika Kambi ya JKT Mgulani iliyopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki katika usaili huo utakaoanza tarehe 10 Agosti 2019 hadi tarehe 14 Agosti 2019 ukisimamiwa na maafisa kutoka Idara ya Uhamiaji.

Aidha, vijana watakaokuwa na sifa wanatakiwa kujitegemea kwa gharama za malazi, chakula na usafiri kwa muda wote watakaokuwa katika usaili.

Sifa ya kujiunga na usaili huo ni kama ifuatavyo:

  • Awe raia wa Tanzania mwenye afya njema kimwili na kiakili.
  • Awe hajawahi kushitakiwa na kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai nchini au nje ya nchi.
  • Mwenye uwezo wa kuzungumza na kuandika lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha zaidi, mwenye uwezo wa kuandika, kuzungumza lugha nyinginezo za kimataifa watapewa kipaumbele kwanza.
  • Mwenye umri wa kuanzia miaka 18 mpaka miaka 30.
  • Awe tayari kuhudhuria na kuhitimu mafunzo ya awali ya askari wa uhamiaji kwa kipindi kisichozidi miezi tisa katika chuo chochote cha kijeshi.
  • Mwenye shahada ya kwanza/ stashahada ya Juu kutoka chuo cha Elimu ya Juu au taasisi inayotambuliwa na Serikali, waombaji wenye shahada ya TEHAMA, Uhandisi mitambo, Umeme, Eletroniki na Mawasiliano ya Umma, Usanifu wa Majengo, Lugha za Kimataifa, Mass Communications/ Journalism, Project Management and Evaluations watapewa kipaumbele.

Vijana wenye sifa wanatakiwa kufika kwenye usaili wakiwa na vitu vifuatavyo:

  • Cheti halisi na nakala moja ya cheti cha kuzaliwa mwombaji.
  • Nakala ya vyeti vya kuhitimu elimu ya darasa la saba, Kidato cha nne, kidato cha sita na shahada ya juu kutoka chuo au taasisi yoyote inayotambuliwa na serikali.
  • Cheti halisi cha kuhitimu Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa na kalamu.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 03 Agosti 2019

Kwa maelezo zaidi tembelea website ya JKT >>>>> USAILI UHAMIAJI

No comments:

Post a Comment